Wanariadha sita (06) kutoka Tanzania wameng’ara katika Mashindano ya mbio ndefu za Marathon za Nagai 2024, yaliyofanyika tarehe 13 Oktoba 2024, jijini Nagai, Yamagata.

Katika mashindano ya Kilomita 42 wanaume, Mwanariadha Charles Boay Sulle ameshinda nafasi ya kwanza kwa kuweka Rekodi ambapo Fabiano Joseph Himindi akishika nafasi ya tatu. Kilomita 42 Wanawake Natalia Elisante Sulle ameshika nafasi ya kwanza.

Katika mbio za Kilomita 21 Wanaume Jumanne Maduhu Ndege ameshika nafasi ya kwanza kwa kuweka Rekodi na Marco Sylvester Monko nafasi ya nne. Kwa upande wa Wanawake Kilomita 21 Neema Salimu Kisuda ameshinda nafasi ya kwanza.

Mashindano ya Nagai Marathon 2024 yameshirikisha wakimbiaji 700 na yamezinduliwa na Meya wa Jiji la Nagai Shigeharu Uchiya na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan Baraka Luvanda, Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe pamoja na Mwanariadha wa zamani Juma Ikangaa ambaye pia ameongoza ujumbe wa wanariadha hao.