Tarehe 17 Julai 2026, Mheshimiwa Anderson Mutatembwa, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan, alipokea ujumbe kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita katika Ofisi za Ubalozi jijini Tokyo.

Ujumbe huo ulifika kwa lengo la kutoa salamu na kuufahamisha Ubalozi kuhusu ziara yao ya mafunzo nchini Japan, inayolenga kujifunza uzoefu katika maeneo ya usimamizi wa usafi na mazingira ya miji, maendeleo ya miundombinu, pamoja na mifumo ya ukusanyaji wa mapato ya mamlaka za serikali za mitaa.

Ujumbe huo uliongozwa na Bw. Yefred Edson Mnyenzi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Bw. Leonard Buhomola Kiganga-Meya wa Halmashauri ya Geita, na  wataalamu kutoka Halmashauri, TARURA, kampuni ya  Luptan Consultancy Co. LTD, ambayo imepata kandarasi ya Mtaalam Mwelekezi wa miradi ya ujenzi wa barabara, pamoja na mwakilishi wa Sky Business and Investment Development Co. Ltd., ambao ni waratibu wa ziara hiyo.