Tarehe 19/07/2026 Mheshimiwa Balozi Anderson Mutatembwa aliipongeza Idara ya Kiswahili iliyopo chini ya Kitivo cha Masomo ya Kigeni cha Chuo Kikuu cha Osaka.
Balozi Mutatembwa alitoa pongezi hizo kwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa Idara hiyo Bi. Keiko Takemura na Uongozi mzima katika Siku ya Maadhimisho ya Miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Idara hiyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kumbukumbu wa Kitivo hicho Kampasi ya Minoo, Jijini Osaka.
Alieleza kuwa kwa kipindi cha miaka 40 Idara hiyo imepiga hatua kubwa katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika ngazi ya Stashahada, Shahada, Uzamili na Uzamivu na kuwa Chuo Kikuu pakee nchini Japan kilichofanikiwa kuitangaza lugha hiyo na utamaduni wa Mtanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla na kuimarisha ushirikiano kati ya Japan na Tanzania ambayo ndiyo chimbuko la lugha hiyo.
Alibainisha kuwa hadi sasa Kiswahili kinatumiwa kama lugha ya mawasiliano na zaidi ya watu milioni 200 Duniani na imetambuliwa kimataifa na UNESCO.
Maadhimisho hayo pia yalihudhiriwa na Naibu Balozi wa Kenya nchini Japan Balozi Aurther Andambi, akiyewahi kuwa Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye sasa na Balozi wa Japan kanda ya Kansai Yasushi Misawa na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan Bi...... Pia walihudhuria Walimu wa Kiswahili tangu ilipoanzishwa Idara hiyo, wahitimu wa tangu mwaka 1986 na wa sasa. Hadi sasa zaidi ya wajapan 800 wamehitimu kwa ngazi mbali mbali katika Idara hiyo.







