Tarehe 26 hadi 28 Novemba 2025, Ubalozi ulishiriki zoezi la ukaguzi na majaribio ya boti mbili za mwendo kasi zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya doria katika eneo lake la ndani maji ya bahari ya Hindi.
Ukaguzi huo ulifanywa na wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Maafa, UNDP ambao ni wafadhili, IRDP na TASAC katika kituo cha “New Japan Marine” Iseshi, Mkoa wa Mie nchini Japan kilipo kiwanda cha YAMAHA MOTORS watengenezaji na wauzaji wa boti hizo.










