Leo, Ubalozi umepokea wanariadha wa Tanzania, Sgt. Alphonce Felix Simbu, Mshindi wa Dunia wa Mbio Ndefu (Marathon) katika Mashindano ya Dunia 2025 yaliyofanyika Tokyo, Japan, pamoja na Cpl. Josephat Joshua Gisemo, wakiwa wameambatana na ujumbe wao.
Mapokezi ya ujumbe huo yalihudhuriwa pia na wawakilishi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Japan (Diaspora), maafisa waandamizi wa Serikali walioko Japan kwa shughuli mbalimbali, pamoja na marafiki wa Tanzania kutoka Japan.
Kwa muda wa saa 2:09:48, Sgt. Simbu aliandika ukurasa wa historia ya Taifa letu, akibeba heshima na hadhi ya Tanzania katika medani ya kimataifa kwa ushindi wake wa kihistoria uliopatikana tarehe 15 Septemba 2025.
Hongera kwa mashujaa wetu wa michezo kwa kutufanya Watanzania wote duniani tuwe na fahari kubwa.



