Tarehe 26 Febuari 2026 ubalozi uliendesha Semina kuhusu Tanzania kwa wanafunzi 79 walihitimu Darasa la Sita katika Shule ya Msingi Komazawa (Komazawa Elementary School) iliyopo Tokyo.
Katika Semina hiyo Afisa Ubalozi Bw. Hosea Chikolongo akisaidiana na Bw. Kazuma Shirai, walielezea Tanzania mahali ilipo, idadi ya watu, vivutio vya utalii na uwekezaji, utamaduni wa mavazi na vyakula. Semina hizo zimekuwa zikifanyika kwa wanafunzi hao wanapohitimu kila mwaka kwa lengo la kupata uelewa wa Tanzania na uzuri wake.


