Leo, tarehe 16 Januari 2026, Mhe. Anderson Mutatembwa, ametembelewa na Bw. Yoshi Nomura, Naibu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa (International Cooperation Bureau) wa KEIDANREN (Japan Business Federation).

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Tanzania na Japan, hususan katika kukuza uwekezaji wa sekta binafsi ya Japan nchini Tanzania. Viongozi hao walijadiliana kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania, mazingira ya biashara, pamoja na mikakati ya kuongeza ushiriki wa kampuni za Kijapani katika miradi ya maendeleo ikiwemo sekta za miundombinu, TEHAMA, viwanda vya uzalishaji, nishati na kilimo.

Aidha, pande hizo zilisisitiza umuhimu wa kuendelea na mawasiliano ya karibu kati ya Ubalozi na Keidanren, ikiwa ni pamoja na kuandaa majukwaa ya biashara na uwekezaji yatakayowezesha wafanyabiashara wa Japan kupata taarifa sahihi na za kina kuhusu Tanzania, pamoja na kuchochea ushiriki wao katika miradi ya kimkakati kwa maendeleo ya Taifa.