Balozi Baraka Luvanda alishuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano “Sister Cities” Kati ya Jiji la Dodoma na Nagai lililopo Mkoa wa Yamagata nchini Japan, tarehe 14 Oktoba 2024.
Utiaji saini ulifanywa na Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe pamoja na Meya wa Jiji la Nagai Shigeharu Uchiya katika sherehe za maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jiji la Nagai Mwaka 1954.
Makubaliano yaliyosainiwa yana lengo la kujenga uhusiano baina ya majiji hayo kwa maslahi ya pande zote mbili ili kukuza ushirikiano wa watu wake katika nyanja za Uendelezaji Majiji hayo, Kutunza Mazingira, Elimu na Utamaduni, Uchumi na Michezo.



