FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO NCHINI JAPAN KWA MWAKA 2027
(JAPANESE GOVERNMENT – MEXT SCHOLARSHIP PROGRAM 2027)
Ubalozi umepokea taarifa ya fursa za ufadhili wa masomo nchini Japan inayotolewa na Serikali ya Japan kupitia Wizara ya Elimu, Utamaduni, Michezo, Sayansi na Teknolojia (Ministry of Education, Culture, Sports, Science and Technology - MEXT) kwa mwaka wa masomo 2027. Ufadhili huo ni kwa masomo ya kada mbalimbali kwa ngazi ya:
i) Shahada ya Kwanza (Undergraduate Studies),
ii) Umahiri (Master’s Degree),
iii) Uzamivu (PhD.) na
iv) Mafunzo ya Ufundi (Specialized Training College).
Taarifa zaidi kuhusu ufadhili ikiwemo, sifa na taratibu za uoambaji zinapatikana kupitia tovuti ya Ubalozi wa Japan nchini Tanzania https://www.tz.emb-japan.go.jp/itpr_en/MEXT2027_00001.html
Maombi yote kuhusu ufadhili huo, yapitie Ubalozi wa Japan nchini Tanzania uliopo Jijini Dar es Salaam, kupitia posta au kuwasilisha ubalozini:
P.O. Box 2577,
Plot No. 1018,
Ali Hassan Mwinyi Rd,
DAR ES SALAAM.
Mwisho wa kutuma maombi hayo ni:
a) tarehe 11 Mei 2026, kwa research participants (Masters na PhD); na
b) tarehe 21 Mei 2026, kwa undergraduate/specialized training college.
Tunashukuru kwa ushirikiano.
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI JAPAN
TOKYO
24 Aprili 2026
