Tarehe 24 Januari 2026 Balozi wa Tanzania nchini Japan Anderson Mutatembwa alitembelea Makumbusho ya Vinyago vya kimakonde (Makonde Art Museum) iliyopo katika mji wa Toba Jimbo la Mie nchini Japan. Makumbusho hiyo ilianzishwa na raia wa Japan Bw.Tsumeo Mizumo ambaye alianza kukusanya Sanaa mbalimbali za vinyago hivyo tangu mwaka 1971.

Makumbusho hiyo ina sanaa mbalimbali za Vinyago vya kimakonde zaidi ya 2000 na ilifunguliwa rasmi mwaka 1991. Pia, kuna sanaa na vifaa vingine vya kiutamaduni vya Tanzania na vya nchi nyingine za Afrika zikiwemo picha za Tingatinga, ala za muziki wa asili na vyombo mbalimbali vya asili vilivyotumiwa majumbani miaka ya nyuma na makabila mbalimbali ya Tanzania.

 

Makonde Art Museum: https://museum.makonde.jp/