Tarehe 05 Febuari 2026 Balozi wa Tanzania nchini Japan Anderson Mutatembwa alitembelea na kuona shughuli za kampuni ya Ukaguzi wa Magari yaliyotumika kabla ya kusafirishwa kwenda nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.
Katika ziara hiyo, Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Prosper Sugai alielezea historia na uzoefu wa kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2007 ambapo imekuwa ikikagua ubora na usalama wa magari yaliyotumika ili kuhakikisha kuwa magari yanayonunuliwa na kusafirishwa kwenda nje ya Japan yanakidhi viwango.
Kampuni ya EAA Company Limited ndiyo iliyopewa dhamana na na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) kufanya kazi ya ukaguzi wa magari na baiskeli zilizotumika zinazonunuliwa na kusafirishwa kwenda Tanzania kwa matumizi.




