Tarehe 19/01/2026 Balozi wa Tanzania nchini Japan alikutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jiji la Nagai lililopo Mkoa wa Yamagata nchini Japan Mheshimiwa Shigeharu Uchita.
Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha uhusiano wa kihistoria baina ya Japan na Tanzania ambapo Jiji hilo limekuwa na ushirikiano na Tanzania kupitia michezo, elimu, utamaduni na uendelezaji Jamii kiuchumi.
Katika mazungumzo yao walikubaliana kuendeleza ushirikiano uliopo kupitia Nagai Marathon, mbio ambazo hufanyika kila mwaka tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017 na kushirikisha wanariadha maarufu kutoka Tanzania.
Aidha, walikubaliana kuendelea kubadirishana uzoefu na ujuzi kwa wanafunzi wa vyuo vya ufundi (VETA) na Nagai Technical High School. Pia Meya Uchiya aliahidi kuwapokea vijana watakaopenda kujifunza Uhandisi katika vyuo vya Japan ambapo Halmashauri yake itakuwa tayari kuwasaidia.
Aidha, walijadiliana namna ya kuanza utekelezaji wa Mkataba wa Makubaliano kati ya Jiji la Nagai na Dodoma “Sister Cities MoU” uliosainiwa Novemba,2024 ulioainisha ushirikiano katika uendelezaji Miji, Mazingira, Elimu na Utamaduni, uchumi na Michezo




