Tarehe 23 Disemba 2025, Balozi Anderson Mutatembwa amefanya mazungumzo na Mhe. KAWAMURA Kenichi, Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii wa Japan (MLIT) anayeshughulikia Miradi ya Kimataifa.
Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye Makao Makuu wa Wizara hiyo jijini Tokyo na yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika maendeleo ya miundombinu, uendelezaji wa rasilimali watu katika sekta ya ujenzi, pamoja na utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa kwa ushirikiano wa pande mbili kupitia MLIT na Shirikisho la JAIDA (Japan- Africa Infrastructure Development Association) ambalo lipo chini ya Wizara hiyo.



