Tarehe 17 Machi 2026, Balozi Anderson Mutatembwa alipokea kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania msaada wa magari matatu ya zimamoto na uokoaji kutoka Japan Firefighters Association. Magari hayo yanatarajiwa kuwasili nchini mwezi Mei 2026, na ni sehemu ya magari matano yatakayotolewa mwaka huu. Kutolewa kwa msaada huo ni utekelezaji wa mpango wa taasisi hiyo wa kutoa jumla ya magari 30 kwa kipindi cha miaka mitano, hadi ifikapo mwaka 2028.

Msaada huu utaimarisha huduma za zimamoto na uokoaji na kuongeza uwezo wa kukabiliana na majanga nchini.