Leo, Darasa la Mafunzo ya Kiswahili liliendelea katika Shule ya Sekondari ya Yoga iliyopo, Yoga, Setagaya, Tokyo, Japan. Darasa hilo huendeshwa na Ubalozi ambapo, Bi. Consolata Luvanda, Mwenza wa Balozi hutoa mafunzo hayo kwa wanajumuiya ya Yoga, mtaa ulipo Ubalozi wa Tanzania @UbaloziJapan jijini Tokyo.
Tangu kuanza kwa darasa hilo limevutia Wajapani wengi kujitokeza na kujifunza lugha ya Kiswahili. Hadi sasa wajapani wapatao 60 wanaendelea kupata mafunzo hayo tangu kuanza kwa darasa hilo mnamo mwezi Aprili mwaka huu.

