Tarehe 24/09/2023 Timu ya mpira wa miguu ya Watanzania waishio Japan Kilimanjaro FC ilicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Guapo FC katika uwanja wa Mizumoto Sports Center Jijini Tokyo. Timu hiyo imechaguliwa tena kushiriki Ligi hiyo kubwa Jijini Tokyo msimu wa 20 mwaka 2023/2024 ambayo ni hatua kubwa. Aidha, Kilimanjaro FC ilishiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza msimu wa 19 mwaka 2022/2023.


