Leo, tarehe 19 Mei 2024, Timu ya Mpira wa Miguu ya Diaspora wa Tanzania nchini Japan inayojulikana kwa jina la The Kilimanjaro KF, imekabidhi Kombe kwa Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda; kufuatia ushindi walioupata wakati wa michuano ya kuwania Kombe la Kimataifa la Samurai Soccer 7’s.

Michuano hiyo ilifanyika tarehe 23 - 24 Machi 2024, jijini Yokohama, Japan na kuandaliwa na Foooty Japan, Chama cha Michezo - Japan; imeshirikisha timu 12 kutoka Mataifa ya Tanzania, Japan, China, Malaysia, Hong Kong, Australia, New Zealand na United Kingdom.
#DIASPORA
#DIPLOMASIA YA MICHEZO

@mfa_tanzania

@MsigwaGerson