Tarehe 19 Navemba, 2023 timu ya wacheza Judo watano (5) kutoka Zanzibar ilishiriki mazoezi ya pamoja ya Judo na timu ya wacheza Judo ishirini na nne (24) wa mji wa Nagai wakiwemo wachezaji wa kimataifa na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Mazoezi hayo yalihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Baraka Luvanda, Viongozi wa mchezo wa Judo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wacheza Judo Mkoa wa Yamagata Bw.Kazuhiko Kuroda na Naibu Meya wa Nagai Bw.Tamaki Saito. Mazoezi hayo ya pamoja yaliandaliwa na Halmashauri ya mji wa Nagai ambapo tarehe 18 November, 2023 Meya wa Nagai  Bw. Shigeharu Uchiya aliwaandalia wachezaji hao chakula cha jioni, hafla iliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa michezo na Maafisa Waandamizi wa Halmashauri hiyo wapatao 38. Wachezaji hao wapo katika Chuo Kikuu cha Juntendo Tokyo tangu mwezi Septemba, 2023 wakihudhuria mafunzo ya mchezo huo chini ya Mwalimu Prof. Morio Suganami.