Tarehe 17 Septemba 2023, Ubalozi wa Tanzania Tokyo uliungana na Watanzania waishio Sydney nchini Australia kumpokea na kumshangilia Mtanzania Gabriel Geay aliyeshiriki mbio ndefu za kimataifa za Sydney Marathon za mwaka 2023. Geay ameshiriki mbio hizo za urefu wa Kilomita 42 zilizoanzia katika Daraja la Habaur View na kuishia katika Jumba la utamaduni la Opera House.
Mbio hizo zilizoshirikisha wanariadha zaidi ya 17,000 duniani, ziliandaliwa na Mamlaka za Mji wa Sydney na kudhaminiwa na kampuni kubwa ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya ASICS.







