Leo, tarehe 01 Oktoba 2024, Ubalozi umepokea ujumbe kutoka Jeshi la Polisi la Tanzania uliongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi Ramadhan Ng’anzi.

Naibu Kamisha Ng’anzi ameongozana na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Deus Sokoni, Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani; na Koplo Rashid Said Abass, Mkaguzi wa Magari na Mtahini wa Madereva.

Ujumbe huu uko nchini Japan kwa kwa ziara ya kikazi ya siku 5 kwa ajili ya kupata mafunzo na kubadilishana uzoefu juu ya ukaguzi wa vyombo vya moto kwa kutumia mitambo ya kisasa.

Aidha, katika ziara hiyo ujumbe huu leo umeweza kuonana na kupata maelezo ya kina juu ya ukaguzi wa magari nchini Japan kutoka kwa Maafisa waandamizi wa Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii ulioongozwa na Bw. Tada Yoshitaka, Mkurugenzi wa Maintenance Service Division, Logistics and Road Transport Bureau.