Tunapenda kuwatangazia Watanzania wote waishio nchini Japan kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Watanzania tarehe 3 Machi 2024 kuanzia saa 4 kamili asubuhi utakaofanyika katika ukumbi wa ubalozi (Tanzania House - Tokyo). Katika mkutano huo wa kikatiba, Mhe. Balozi ataongea na watanzania wote waishio Japan, kupitia taarifa za fedha za Jumuiya, kupitisha Katiba Mpya ya Jumuiya, kujadili muelekeo na Dira ya Jumuiya ya Watanzania walioko Japan, ya mwaka 2024/25.
Baada ya Mkutano huo, kutakua na chakula cha pamoja cha kuukaribisha mwaka mpya itakayoambatana na burudani kadhaa kabla ya kutawanyika. Tunatoa wito kwa kila Mtanzania aliye Japan kushiriki kikamilifu siku hiyo muhimu. Karibu tuijenge Jumuiya yetu. Upatapo ujumbe huu, mjulishe na kumuhimiza mwingine.
NB: Kutokana na maandalizi ya chakula (lunch) na vinywaji, tunaomba uthibitishe ushiriki wako kwa kuandikisha jina lako kwenye mkeka wa ushiriki wa mkutano kwa Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Japan.
ASANTE.
