Mhe. Mary Majaliwa akiwa na wajumbe wengine waalikwa wa Mkutano wakati wa hafla ya ukaribisho iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan, tarehe 28 Novemba 2022
Mhe. Mary Majaliwa pamoja na Mhe. Balozi Baraka Luvanda wakifuatilia Mkutano, tarehe 29 Novemba 2022
Mhe. Mary Majaliwa akipanda mti wa kumbukumbu kwenye eneo la Uhifadhi wa Asili la Minuma Nature Park, Tokyo kama ishara ya kukabiliana na majanga na mabadiliko ya tabianchi, tarehe 30 Novemba 2022
Mhe. Mary Majaliwa akiwasilisha mada kuhusu Tanzania kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Misonokita, Tokyo tarehe 30 Novemba 2022
Mhe. Mary Majaliwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Baraka Luvanda na waandaji wa Mkutano
Mhe. Mary Majaliwa akiwa na Wenza wengine wa Viongozi wa Nchi za Afrika mara baada ya kusaini Tamko la Pamoja (Joint Declaration) la Ushirikiano katika usalama wa chakula na upatikanaji wa maji safi na salama

Mhe. Mary Majaliwa, Mwenza wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshiriki kwenye Mkutano wa Kwanza wa Kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Wanawake wa Nchi za Asia - Pasifiki na Afrika (APA Summit) uliofanyika tarehe 28 Novemba – 1 Desemba 2022 Tokyo, Japan. Mkutano huo uliandaliwa kwa ushirikiano wa Wabunge Wastaafu wa Bunge la Japan pamoja na Serikali ya Japan, kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan. 

Mkutano huo uliwalenga zaidi Wenza wa Viongozi Wakuu wa Nchi zilizopo Asia, Pasifiki na Afrika, ukiwa na lengo la kujadili usalama wa chakula kwa watoto wanaoishi katika nchi hizo hususan, kwa kuzingatia madhara ya kiuchumi yaliyotokana na mabadiliko ya tabia nchi, athari za kivita pamoja na kuenea kwa UVIKO - 19 duniani.

Wakifungua mkutano huo, katika hotuba zao Wenyeviti Wenza wa mkutano, Bi. Seiko Hashimoto ambaye pia ni Mjumbe wa Chemba ya Juu ya Bunge (House of Councillors) na Bi. Fukuyo Nakamori, ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Bunge la Japan walieleza kuwa lengo la mkutano huo ni kujadiliana kuhusu usalama wa chakula kwa watoto wanaoishi katika nchi za Afrika, Pasifiki na Asia. Walieleza kuwa kwa kuzingatia madhara ya kiuchumi yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi, janga la UVIKO 19 pamoja na athari za kivita duniani, hali ya upatikanaji wa chakula cha kutosha imekuwa ni changamoto kwa jamii nyingi. Hivyo, walitumia fursa hiyo kutoa wito kwa nchi za ukanda wa Asia – Pasifiki na Afrika kushirikiana katika kukabiliana na changamoto hizo katika kuhakikisha kunakuwa na usalama wa chakula pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama.

Ufunguzi wa mkutano ulihusisha mawasilisho ya hotuba mbalimbali kutoka kwa wenza wa viongozi ambapo, Mhe. Mary Majaliwa alipata fursa ya kuelezea namna Tanzania inavyotekeleza mikakati mbalimbali ya kuhakikisha usalama wa chakula na kukabiliana na UVIKO-19 pamoja na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Alitaja miongoni mwa hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imekuwa ikizichukua katika kuhakikisha usalama wa chakula katika   jamii ya watanzania kuwa ni pamoja na kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya kilimo ikiwemo, ya umwagiliaji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi; kuzinduliwa kwa kampeni ya kitaifa ya lishe bora  pamoja na kutoa kipaumbele kwenye sekta ya kilimo kwa kuiongezea bajeti ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo; na kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili kuwezesha uwekezaji kwenye sekta ya kilimo kwa kuhakikisha uzalishaji wa chakula unafanyika kwa kiwango cha juu. 

Mkutano ulihitimishwa kwa kusainiwa kwa Tamko la Pamoja (Joint Declaration) ambalo ni msingi wa makubaliano ya kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi husika kupitia wenza wa viongozi wakuu wa nchi hizo katika kuhakikisha usalama wa chakula kwa watoto na pia kujenga mfumo wa ushirikiano wa pamoja wakati wa maafa. 

Mkutano huo wa kwanza wa aina yake ulihudhuriwa na wenza wa viongozi wakuu wa nchi za Bara la Afrika zikiwemo, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Gambia, Malawi, Uganda, Zimbabwe na Tanzania; na umekuwa dira sahihi kwa mikutano mingine ijayo kwa kuweka misingi ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi; kujihakikishia usalama wa chakula na maji safi na salama hususan, kwa watoto; pamoja na kumwezesha mwanamke kukua kiuchumi ili aweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo.

  • Mhe. Mary Majaliwa akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano (APA Summit), tarehe 28 Novemba 2022Mhe. Mary Majaliwa akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano (APA Summit), tarehe 28 Novemba 2022
  • Mhe. Mary Majaliwa kwenye picha ya pamoja na Wenza wa Viongozi walioshiriki Mkutano wa Kwanza wa Kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Wanawake wa Nchi za Asia - Pasifiki na Afrika (APA) uliofanyika tarehe 28 Novemba – 1 Desemba 2022 Tokyo, JapanMhe. Mary Majaliwa kwenye picha ya pamoja na Wenza wa Viongozi walioshiriki Mkutano wa Kwanza wa Kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Wanawake wa Nchi za Asia - Pasifiki na Afrika (APA) uliofanyika tarehe 28 Novemba – 1 Desemba 2022 Tokyo, Japan