Tarehe 22 Oktoba 2024, Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda amewapokea Ubalozini, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Prof. Abel Makubi.
Viongozi hao wapo nchini Japan kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha ushirikiano na Serikali na taasisi za Japan kwenye masuala ya tiba, sayansi na elimu ya tiba.



