Leo, tarehe 01 Julai 2024, Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda aliwapokea Ubalozini, viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Wanaosoma Japan “The Association of Tanzanian Students in Japan – TSJ”; na kufanya nao mazungumzo.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walitoa shukrani kwa Balozi Luvanda ambaye ni Mlezi wa Jumuiya hiyo kwa namna wanavyopata ushirikiano kutoka ubalozini kuhusiana na masuala mbalimbali. Walieleza pia mikakati waliyonayo ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya fursa za masomo kwa watanzania nchini Japan, tafiti pamoja na programu za kubadilishana uzoefu wa wataalam wa sekta mbalimbali kutoka Japan.

Kwa upande wake, Balozi Luvanda aliwashukuru viongozi hao kwa mipango mizuri waliyonayo ambayo kwa kiasi kikubwa inaendana na utekelezaji wa majukumu ya Ubalozi; na kuwaahidi ushirikiano wa Ubalozi wa muda wote.