Tarehe 5 Novemba 2023, Timu ya Mpira wa Miguu ya Diaspora wa Tanzania waliopo Japan (The Kilimanjaro FC) ilishiriki katika mechi za kirafiki na timu nyingine mbili za wanadiaspora waliopo Japan. Mechi hizo zilichezwa kwa mnasaba wa kudumisha urafiki, udugu miongoni mwa wanadiaspora pamoja na kulinda na kujenga afya bora..

Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda pamoja na maafisa wengine wa Ubalozi walishiriki katika kuishangilia na kuihamisha The Kili FC.

Balozi Luvanda ni Mlezi wa The Kili FC. Aidha, Balozi wa Hiari wa Utalii wa Tanzania, Bwana Nicholaus Reynolds, almaarufu  “Bongozozo”alishiriki bega kwa bega kuishangilia na kuihamasisha, hali iliyoifanya timu hiyo kuibuka mshindi kwa kushinda jumla ya  mechi nne (04) kati ya mechi sita (06) zilizochezwa, kushindwa mechi moja (01) na sare mechi moja (01)..

Bongozozo yuko katika ziara ndefu ya kikazi katika Bara la Asia ambapo, kabla ya kuja Japan alitembelea Ufilipino, Cambodia, Indonesia, Singapore, Thailand na Taiwan.