Tarehe 06/08/2023 Balozi Baraka Luvanda aliungana na Mabalozi wengine wapatao mia moja arobaini wanaoziwakilisha nchi zao nchini Japan katika kumbukizi ya miaka 78 tangu ulipotokea mlipuko wa Bomu la nyukilia katika Jiji la Hiroshima mwaka 1945. Hafla hiyo ilifanyika katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya Makumbusho ya Amani tangu kutokea kwa mlipuko huo. Wageni mbalimbali pamoja na wakazi wa Jiji la Hiroshima walijitokeza wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Japani Mheshimiwa Fumio Kishida.

  • Balozi Baraka Luvanda akiweka maua mbele ya kaburi walimozikwa waathirika wengi wa mlipuko wa Nyuklia tarehe 06/08/1945.Balozi Baraka Luvanda akiweka maua mbele ya kaburi walimozikwa waathirika wengi wa mlipuko wa Nyuklia tarehe 06/08/1945.
  • Masalia ya jengo (Dome) kutokana na mlipuko wa bomu kwenye eneo la biashara na viwanda.Masalia ya jengo (Dome) kutokana na mlipuko wa bomu kwenye eneo la biashara na viwanda.
  • Balozi Baraka Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa Wahanga wa Bomu la Nyukilia na mabalozi wengine.Balozi Baraka Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa Wahanga wa Bomu la Nyukilia na mabalozi wengine.
  • Balozi Baraka Luvanda aliyeambatana na Afisa Ubalozi Bw. Hosea Chikolongo wakiwasha mishumaa pembeni mwa mto ambamo miili ya watu wengi ilionekana ikielea baada ya mlipuko.Balozi Baraka Luvanda aliyeambatana na Afisa Ubalozi Bw. Hosea Chikolongo wakiwasha mishumaa pembeni mwa mto ambamo miili ya watu wengi ilionekana ikielea baada ya mlipuko.
  • Mheshimiwa Balozi Luvanda akiwasikiliza na kujadiliana na wanafunzi wa shule waliowasilisha ujumbe wa amani Duniani ikiwa ni sehemu ya Kumbukizi hiyo.Mheshimiwa Balozi Luvanda akiwasikiliza na kujadiliana na wanafunzi wa shule waliowasilisha ujumbe wa amani Duniani ikiwa ni sehemu ya Kumbukizi hiyo.