Kampuni ya ITO EN LTD, kampuni tanzu ya Tully’s Co. Ltd., inayomiliki migahawa maarufu ya Tully’s Coffee, leo tarehe 14 Machi 2024 jijini Tokyo, imezindua aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania, nchini Japan. Aina hizo za kahawa ya Tanzania ni TULLY’s COFFEE BARISTA BLACK KILIMANJARO; TULLY’S COFFEE MY HOME BLACK KILIMANJARO; na TULLY’S COFFEE BARISTA ROAST COLD BREW – KILIMANJARO BLEND. Kahawa hizo ni kutoka maeneo ya Tarime, mkoani Arusha na mashamba ya GDM yaliyoko Mbozi mkoani Mbeya. 
Zoezi hilo la uzinduzi lilifanyika katika Ubalozi wa Tanzania, jijini Tokyo na kuongozwa na Mheshimiwa Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini Japan pamoja na Bw. Osamu Aizawa, Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN aliyeambatana na wawakilishi wa kampuni hiyo na Kampuni ya Tully’s Coffee. 
Uzinduzi huo ulipambwa na zoezi la uonjaji wa kahawa ya Tanzania iliyozinduliwa ambalo, lilishirikisha wataalam wa kahawa (baristas) wapatao 30 wa maeneo mbalimbali nchini Japan.  
Kampuni ya ITO EN Ltd., ni kampuni inayoongoza kwa biashara ya vinywaji nchini Japan ambayo, ni kampuni tanzu ya Tully’s Coffee inayomiliki migahawa ya kahawa takriban 700 nchini Japan na imejipatia umaarufu mkubwa katika biashara ya uuzaji wa kahawa za aina mbalimbali duniani. Kahawa ya Tanzania iliyozinduliwa ni kutoka Mashamba ya kahawa ya GDM (GDM Farms) yaliyoko Mbozi mkoani Mbeya. Hii ni mara ya pili, kwa Kampuni ya Tully’s kuzindua kahawa ya Tanzania katika migahawa yake, uzinduzi kama huu ulifanyika pia mwaka jana mwezi Juni na Agosti, kwa aina ya GDM full washed, GDM natural na Tarime Coffee. 
Kuzinduliwa kwa aina nyingine tatu mpya za kahawa nchini Japan, kunaendelea kupandisha zaidi uhakika wa soko la kahawa ya Tanzania, Japan ambayo imejizolea umaarufu mkubwa kwa ubora na radha ya aina yake na kupelekea kupewa jina maarufu la kibiashara la Kilimanjaro Coffee. Kilimanjrao Coffee ni miongoni mwa brand tatu duniani zinazopendwa zaidi Japan; na jina hilo hutumika nchini humo kwa kahawa zinazozalishwa Tanzania pekee, kwa kutambua kivutio kikubwa cha Mlima Kilimanjaro uliopo nchini Tanzania. 
Tanzania inasifika Japan kwa kutoa kahawa bora aina ya Arabica (Arabica laini - full washed na Arabica ngumu - natural) inayolimwa katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mara, Tanga, Morogoro, Njombe, Iringa, Katavi, Rukwa, Ruvuma, Kigoma, Songwe na Mbeya; na kahawa ya Robusta inayolimwa mkoani Kagera. 
Akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo, Balozi Baraka Luvanda alizihakikishia kampuni za Japan, uwepo wa mazingira wezeshi ya biashara na hata uwekezaji wanapoamua kuwekeza katika kilimo au sekta nyinginezo. Amelitaja kuwa zao la kahawa ni miongoni mwa mazao ya kimkakati nchini ambalo, linatumika kibiashara kwa kulipatia Taifa pato kubwa kwa mauzo mengi ya kigeni. Akitolea mfano wa Japan, alieleza kuwa kwa mwaka, Tanzania inauza kahawa yake Japan kwa wastani wa asilimia 33 ya kahawa inayolimwa nchini, ambayo ni sawa na wastani wa kilogramu million 15 (tani 15,000) ya kahawa yote ya Tanzania inayouzwa nchini Japan. Takwimu hizo zinaiweka Japan kuwa mnunuzi mkubwa na namba moja (1) wa kahawa inayolimwa nchini.
Aidha, Balozi Luvanda alielezea juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo kwa kuwekeza katika miradi ya muda mrefu na mifupi pamoja na maeneo ya msingi ya kutatua changamoto za kilimo kuanzia shambani hadi sokoni ili kujihakikishia uhakika wa chakula, kulisha wengine kibiashara duniani, na pia wakulima kujipatia kipato cha kutosha ili kupunguza umaskini.
Balozi Luvanda pia alihamasisha ushiriki wa wadau wa kahawa nchini katika Maonesho ya Kimataifa ya Kahawa ya Mwaka 2024 (World Specialty Coffee Conference and Exhibition 2024) yatakayofanyika jijini Tokyo mwezi Oktoba 2024, ambayo yanaratibiwa na Ubalozi kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania. Tanzania ilishiriki kikamilifu katika Maonesho hayo mwaka 2023; na manufaa yake yameonekana.

IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI JAPAN
TAREHE 14 MACHI 2024

  • Balozi Baraka Luvanda kwenye picha ya pamoja na Bw. Osamu Aizawa, Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN na wawakilishi wa Kampuni ya Tully’s Coffee, wakitambulisha kahawa za Tanzania  katika hafla ya uzinduzi wa kahawa hizo nchini JapanBalozi Baraka Luvanda kwenye picha ya pamoja na Bw. Osamu Aizawa, Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN na wawakilishi wa Kampuni ya Tully’s Coffee, wakitambulisha kahawa za Tanzania katika hafla ya uzinduzi wa kahawa hizo nchini Japan
  • Mheshimiwa Baraka Luvanda akitoa salamu za ukaribisho katika hafla ya uzinduzi wa aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania zilizozinduliwa na Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee nchini JapanMheshimiwa Baraka Luvanda akitoa salamu za ukaribisho katika hafla ya uzinduzi wa aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania zilizozinduliwa na Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee nchini Japan
  • Bw. Osamu Aizawa, Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN akitoa salamu za ukaribisho katika hafla ya uzinduzi wa aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania, zilizozinduliwa na Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee nchini JapanBw. Osamu Aizawa, Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN akitoa salamu za ukaribisho katika hafla ya uzinduzi wa aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania, zilizozinduliwa na Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee nchini Japan
  • Mtaalam wa Kahawa (barista) wa Kampuni ya Tully’s Coffee akielezea maeneo inapolimwa kahawa ya Tanzania iliyozinduliwa nchini Japan na Kampuni ya ITO EN na Tully’s CoffeeMtaalam wa Kahawa (barista) wa Kampuni ya Tully’s Coffee akielezea maeneo inapolimwa kahawa ya Tanzania iliyozinduliwa nchini Japan na Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee
  • Mtaalam wa Kahawa (barista) wa Kampuni ya Tully’s Coffee akielezea utayarishaji wa kahawa  katika hafla ya uzinduzi wa aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania kwa Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee za nchini JapanMtaalam wa Kahawa (barista) wa Kampuni ya Tully’s Coffee akielezea utayarishaji wa kahawa katika hafla ya uzinduzi wa aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania kwa Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee za nchini Japan
  • Mtaalam wa Kahawa (barista) wa Kampuni ya Tully’s Coffee akielezea utayarishaji wa kahawa  katika hafla ya uzinduzi wa aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania kwa Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee, nchini JapanMtaalam wa Kahawa (barista) wa Kampuni ya Tully’s Coffee akielezea utayarishaji wa kahawa katika hafla ya uzinduzi wa aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania kwa Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee, nchini Japan
  • Bw. Osamu Aizawa, Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN, akitambulisha aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania  katika hafla ya uzinduzi wa kahawa hizo, nchini JapanBw. Osamu Aizawa, Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN, akitambulisha aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania katika hafla ya uzinduzi wa kahawa hizo, nchini Japan
  • Semina maalum kuhusu kahawa ya Tanzania kitolewa kwa washiriki waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa aina tatu za kahawa ya Tanzania zilizozinduliwa na Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee, nchini JapanSemina maalum kuhusu kahawa ya Tanzania kitolewa kwa washiriki waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa aina tatu za kahawa ya Tanzania zilizozinduliwa na Kampuni ya ITO EN na Tully’s Coffee, nchini Japan
  • Balozi Baraka Luvanda kwenye picha ya pamoja na Bw. Osamu Aizawa, Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN, wakitambulisha kahawa za Tanzania  katika hafla ya uzinduzi wa kahawa hizo, nchini JapanBalozi Baraka Luvanda kwenye picha ya pamoja na Bw. Osamu Aizawa, Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN, wakitambulisha kahawa za Tanzania katika hafla ya uzinduzi wa kahawa hizo, nchini Japan