Tanzania inashiriki kwenye Mkutano wa Tano Maandalizi (International Participants Meeting - IPM) ya Maonesho ya Dunia 2025, yajulikanayo “EXPO 2025 Osaka, Kansai, Japan”, unaofanyika tarehe 15 - 17 Januari 2025, mjini Himeji, Japan. Mkutano huo una hudhuriwa na washiriki wapatao 600 kutoka nchi takriban 160 duniani, ukiwa na lengo la kutoa taarifa kuhusu uandaaji wa mabanda ya Maonesho kwa washiriki; na kujadili hatua za maandalizi ya Maonesho husika kutoka kwa waandaaji pamoja na nchi washiriki.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah aliyeambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bi. Latifa M. Khamis pamoja na Maafisa kutoka Balozi wa Tanzania nchini Japan.
Maonesho ya EXPO 2025 yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 13 Aprili hadi 13 Oktoba, 2025 Osaka, Kansai, Japan katika kisiwa cha Yumeshima kwa lengo la kutangaza fursa mbalimbali zipatikanazo duniani.