📍AUSTRALIA NA NEW ZEALAND
🟡HUDUMA YA KIKONSELI

Ubalozi wa Tanzania nchini Japan ambao pia unaiwakilisha Tanzania katika nchi za Australia, New Zealand na Papua New Guinea unaendesha zoezi la kukamilisha maombi ya Pasi za kusafiria kwa Watanzania (Diaspora) wanaoishi katika nchi hizo. Zoezi linafanyika katika miji ya Auckland (New Zealand), Perth, Melbourne na Sydney nchini Australia. Zoezi hilo linapata mwitikio mzuri kwa Watanzania walioomba huduma hiyo. Aidha, Watanzania wengine wenye uhitaji wa huduma hii wanasisitizwa kuendelea kujitokeza katika vituo vilivyotangazwa.

Zoezi hili lilianza tarehe 12 na linatarajiwa kuhitimishwa tarehe 22 Mei 2024.