Leo tarehe 7 Septemba 2022, saa 5.00 asubuhi, Balozi Baraka H. Luvanda, amezungumza na vyombo vya habari vya Tanzania kupitia mtandao wa Zoom uliokuwa mubashara kutokea Tokyo, Japan. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuelezea matokeo ya Mkutano wa Nane wa Kilele wa Ushirikiano wa Kimaendeleo kati ya Japan na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (8th Tokyo International Conference on African Development – TICAD 8) pamoja na namna Tanzania itakavyoweza kunufaika na yaliyoafikiwa katika mkutano huo.