MPANGO WA KUKUSANYA MAOMBI YA HATI ZA KUSAFIRIA KWA WATANZANIA WAISHIO AUSTRALIA NA NEW ZEALAND

Ubalozi wa Tanzania Tokyo, unapenda kuwajulisha kuwa muda wa kupokea maombi yenu ya Hati za kusafiria umeongezwa hadi tarehe 14 Machi, 2023. Hii ni kutoa nafasi kwa Watanzania wengi zaidi waliopo katika nchi tajwa kukamilisha maombi yao na kuyatuma Ubalozini. Ubalozi unakumbusha hatua za kufuata kama ifuatavyo:-

HATUA YA KWANZA

VIAMBATA WAKATI WA KUJAZA FOMU MTANDAONI www.immigration.go.tz

  1. Cheti cha kuzaliwa cha mhusika
  2. Cheti cha kuzaliwa cha baba au mama wa mwombaji au afidavit kama mhusika amezaliwa kabla ya mwaka 1981
  3. Hati (pasipoti) ya kusafiria iliyoisha muda wake 
  4. Kibali (residence permit) cha kuishi katika nchi husika
  5. Barua ya kuomba pasipoti
  6. Picha moja ili uitumie wakati wa kujaza maombi ya pasipoti katika mtandao

HATUA YA PILI

Baada ya kukamilisha kuandaa mahitaji hapo juu, mwombaji atatakiwa kujaza maombi ya pasipoti mwanzo mpaka analipia ombi lake.

HATUA YA TATU

Mwombaji atatakiwa kutumia control number aliyoipata kufanya malipo kwa njia ya mtandao. Namna ya kulipia ingia katika mtandao: https://epay.gepg.go.tz/ fanya malipo mwanzo mpaka mwisho kwa kuingiza control number utakayopewa.

HATUA YA NNE

Muombaji akisha jaza fomu atatakiwa kupakua (Download) fomu yake na kujaza maeneo yote yaliyo wazi. Aidha, baada ya kujaza fomu hiyo atatakiwa kuituma Ubalozi wa Tanzania Tokyo ili maombi hayo yaweze kufanyiwa kazi na kuingizwa kwenye mfumo.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:

  1. Kila mwombaji ajaze fomu ya maombi na kuituma ubalozini kwa barua pepe tokyo@nje.go.tz kabla ya tarehe 14/03/2023 bila kukosa.
  2. Mwombaji ambaye hatajaza fomu yake na kuituma Ubalozini hataweza kuhudumiwa kipindi cha kuchukuliwa alama za vidole na upigaji picha.
  3. Sehemu ya 9 SHUHUDA WA MUOMBAJI isijazwe. Hii ni sehemu ambayo Ubalozi utatakiwa kujaza na kugonga muhuri. Mwombaji ajaze sehemu ya 4 na sehemu ya 7 za fomu baada ya kuipakua.

 

MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI HAYO UBALOZINI NI TAREHE 14/03/2023