Leo, tarehe 4 Julai 2024, Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda amewasilisha mada maalum kuhusu Tanzania, Historia ya Lugha ya Kiswahili na Utamaduni wake kwa wanafunzi wanaosoma Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Sophia, kilichopo Tokyo.
Mhe. Balozi Luvanda ametoa wasilisho hilo ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani nchini Japan ambayo, kilele chake itaadhimishwa duniani kote mnamo tarehe 7 Julai.
Balozi Luvanda pia alipata wasaa wa kufanya mazungumzo na Mkuu wa Chuo cha Sophia, Prof. Yoshiaki Terumichi yaliyolenga ushirikiano kati ya chuo hicho na vyuo vikuu vya Tanzania katika maeneo ya Lugha ya Kiswahili, tafiti za kisayansi na program za kujenga na kubadilishana uzoefu.
Tunashukuru Chuo Kikuu cha Sophia na vyuo vikuu vingine nchini Japan vinavyofundisha Lugha ya Kiswahili kwa kuitangaza na kukuza lugha hii adhimu, nchini Japan.