Leo, tarehe 24 Septemba 2024, Balozi Baraka Luvanda amepokea kwa mara ya kwanza shehena la mananasi yaliyokaushwa kutoka Tanzania – Bagamoyo (Kimele, Mapinga) kupitia Kampuni ya Taishin Co. Ltd., ya Japan. Mapokezi hayo yamefanyika katika Bandari ya Tokyo kwenye hifadhi za bandari hiyo za Kawanishi (Kawanishi Warehouse) jijini Tokyo.
Shehena hiyo imewasili nchini Japan kwa ajili ya kutambulisha zao hilo katika soko la Japan ambalo, linatarajiwa kuanza kuuzwa kwenye supermarkets za TOMIZAWA na LIFE CORPORATION zilizopo Japan kote.
Kampuni ya Taishin ya Japan ina ubia na Kampuni ya Elven Agri ya Tanzania katika kuleta zao hilo nchini Japan. Hii ni fursa kubwa kwa nchi yetu na wakulima wa zao hili katika kulifikia soko la Japan. Ubalozi unatoa shukrani kwa Kampuni hizo kwa ushirikiano wao katika kufanikisha hatua hii.