Tarehe 17 Oktoba 2024, Ujumbe wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Bw. Primus Kimaryo, ulipotembelea Ofisi za Ubalozi jijini Tokyo na kupokelewa na Mhe. Balozi Baraka Luvanda.

Ujumbe huo ulikuwa Japan, kuanzia tarehe 9 hadi 16 Oktoba 2024, kwa KAMPENI MAALUM YA KUTAFUTA MASOKO NA WAWEKEZAJI WA KAHAWA YA TANZANIA iliyojumuisha ushiriki kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kahawa Japan 2024 (SCAJ 2024), Semina Maalum ya Uhamasishaji kuhusu Kahawa ya Tanzania na mikutano ya ubia na Serikali ya Japan, mashirika na makampuni yanayojishughulisha na kahawa nchini Japan.