Tarehe 8 Juni 2024, Kampeni ya Kutangaza na Kuhamasisha Fursa za Uwekezaji za Tanzania nchini Japan iliyoongozwa na Mheshimiwa Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini Japan, pamoja na Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, imehitimishwa kwa mafanikio makubwa kwa kuvutia na kuhamasika kampuni za Japan kuwekeza nchini.
Kampeni hiyo iliyofanyika kuanzia tarehe 27 Mei 2024, imehusisha uwepo wa Makongamano ya Uwekezaji kwa makampuni na wawekezaji waliopo kwenye miji mikubwa ya Japan ya Tokyo, Osaka, Shizouka na Chiba. Kampeni hiyo pia ilijumuisha Semina Elekezi kwa Watendaji Wakuu na Wamiliki wa Makampuni ya KEIZA DOYUKAI na KEIDANREN, Taasisi ya Japan kwa Maendeleo ya Miundombinu ya Afrika (JAIDA) pamoja na Jumuiya ya Watanzania (DIASPORA) waliopo Japan.
Aidha, kulifanyika mikutano ya ana kwa ana na taasisi za Serikali ya Japan ikiwemo, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Shirika la Biashara za Nje la Japan (JETRO), pamoja na kampuni mbalimbali zinazohusika na kilimo, ujenzi wa miundombinu na majengo, usafirishaji, afya, madini, nishati, uchumi wa buluu, na viwanda. Miongoni mwa kampuni hizo ni pamoja na TOPPAN HOLDINGS, TOYOTA TSUSHO, SUMITOMO, EARTH PHARMACEUTICALS, YAMAHA, SUZUKI, KIKKOMAN, AXCEL Africa, SAGRI, ROHTO PHARMACEUTICAL, YOKOGAWA Electric na DAIKIN yenye ubia na Kampuni ya Baridi Baridi inayoendesha shughuli zake nchini Tanzania.
Vilevile, Ujumbe wa Tanzania ulifanya Mkutano na Wabunge wa Umoja wa Afrika – Japan Parliamentary Friendship Association, katika majengo ya Bunge la Japan, jijini Tokyo; na Mhadhara wa Uwekezaji kwa wanafunzi pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha SOPHIA kilichopo jijini Tokyo. Chuo Kikuu SOPHIA ni miongoni mwa vyuo vikuu vya Japan vyenye Programu ya Masomo ya Afrika (Africa studies) na Lugha ya Kiswahili.
Kutokana na Kampeni hiyo, wawekezaji wa Japan wapatao 100, wanatarajiwa kuitembelea Tanzania mnamo mwezi Oktoba, mwaka huu (2024) kwa ajili ya majadiliano zaidi na kuhitimisha mazungumzo na kampuni na taasisi za sekta husika nchini Tanzania. Aidha, JICA na TIC zimekubaliana kubadilishana wataalamu ili kuchochea na kuhamasisha uwekezaji zaidi kutoka Japan.
Kampeni hii ya aina yake iliyokuwa maalum kwa kuhamasisha uwekezaji wa Japan imeandaliwa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP).
Japan ni miongoni mwa nchi zilizowekeza katika viwanda na kampuni zinazofanya shughuli mbalimbali kwa kiwango kikubwa nchini Tanzania ambazo, zimeajiri watanzania wengi na kuwa chanzo muhimu cha uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nchi za nje (Foreign Direct Investment - FDI). Miongoni mwa kampuni hizo za Japan zilizopo nchini ni pamoja na; JAPAN TOBACCO yenye ubia na Kiwanda cha Sigara Tanzania (TCC); SUMITOMO Chemicals yenye ubia na Kiwanda cha A to Z kinachotengeneza chandarua kilichopo Arusha; TANJA Ltd iliyowekeza kwenye mashamba ya kahawa – Tarime; Matoborwa Company inayojishughulisha na ukaushaji wa matunda kilichopo Dodoma; Baridi Baridi Company inayojishughulisha na viyoyozi (AC); na kampuni nyinginezo.
IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI JAPAN
8 JUNI 2024
TOKYO
タンザニア投資プロモーションミッションin Japan
2024年5月27日‐6月8日
2024年6月8日、バラカ・ルヴァンダ駐日タンザニア大使およびジレッド・テリタンザニア投資センター(TIC)総裁率いるタンザニアへの投資誘致キャンペーンが成功裏に終わりました。本キャンペーンでは多くの日本企業の皆さまにタンザニアへの投資に関心をお寄せいただきました。
2024年5月27日から6月8日まで行われたキャンペーン期間中、東京、大阪、静岡、千葉といった主要都市にて企業や投資家向けの様々なカンファレンスが開催されました。経済同友会、日本経済団体連合会(経団連)、アフリカ・インフラ協議会(JAIDA)や在日タンザニア人コミュニティとも個別に会合が行われました。
その他にも国際協力機構(JICA)、日本貿易振興機構(JETRO)をはじめ農業、インフラ建設、運輸、医療、ブルーエコノミーなど多様な分野の日本企業ともミーティングが行われました。対面ミーティングが実現した企業はTOPPANホールディングス、豊田通商、住友商事、アース製薬、ヤマハ発動機、スズキ、キッコーマン、アクセルアフリカ、サグリ、ロート製薬、横河電機、タンザニアでバリディバリディとのジョイントベンチャーを展開するダイキン工業などです。
また衆議院議員会館にて日本アフリカ連合友好議員連盟議員とも会合が行われたほか、上智大学にてタンザニアについての一般公開講座がオンライン・対面の両方で開催されました。
その結果、およそ100名の投資家が今年10月に日本からタンザニアを訪れ関連企業や当局と協議を進める運びとなりました。加えて、JICAとTICは日本からの投資を促進するため専門家の交換プログラムを進めることに同意しました。
今回の日本からの投資促進を目的としたプログラムは駐日タンザニア大使館、タンザニア投資センター、国連工業開発機関(UNIDO)および国連開発計画(UNDP)のコラボレーションにより開催されました。
結びに、日本はタンザニアにとって重要な投資家であり、これまでにも多くの日本企業が我が国に投資し雇用創出してきました。主要な例としては日本たばこ産業とタンザニア・シガレット社(TCC)のジョイントベンチャー、アルーシャの住友化学とA-to-Zファクトリーによる蚊帳のジョイントベンチャー、タリメのコーヒー農園に投資するTANJA、ドドマにてフルーツ加工に参入しているマトボロワ、エアコン事業のバリディバリディなどがあります。
2024年6月8日
駐日タンザニア大使館
Picha ya pamoja na Watendaji wa Kampuni ya TOPPAN kwenye Makao Makuu ya kampuni hiyo, jijini Tokyo, Japan, tarehe 27 Mei 2024
Picha ya pamoja na Watendaji wa Kampuni ya TOYOTA TSUSHO kwenye Makao Makuu ya kampuni hiyo, jijini Tokyo, Japan, tarehe 27 Mei 2024
Mazungumzo na Watendaji Wakuu wa Kampuni ya SUMITOMO, jijini Tokyo, Japan, tarehe 27 Mei 2024.
Picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Shirika la Biashara za Nje la Japan (JETRO), kwenye Makao Makuu ya JETRO, tarehe 27 Mei 2024.
Mazungumzo na Watendaji Wakuu na Wamiliki wa Makampuni ya KEIZA DOYUKAI, tarehe 28 Mei 2024.
Wawakilishi wa kampuni za jijini Tokyo, kwenye Semina Elekezi ya Uwekezaji wakati wa Kampeni ya Kuhamasisha na Kutangaza Fursa za Uwekezaji za Tanzania nchini Japan, tarehe 28 Mei 2024.
Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwenye Semina Elekezi ya Uwekezaji jijini Tokyo wakati wa Kampeni ya Kuhamasisha na Kutangaza Fursa za Uwekezaji za Tanzania nchini Japan, tarehe 28 Mei 2024.
Semina Elekezi ya Uwekezaji jijini Tokyo wakati wa Kampeni ya Kuhamasisha na Kutangaza Fursa za Uwekezaji za Tanzania nchini Japan, tarehe 28 Mei 2024.
Mhadhara wa Uwekezaji kwa wanafunzi pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha SOPHIA kilichopo jijini Tokyo, tarehe 28 Mei 2024.
Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda na Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania wakiongoza majadiliano wakati wa Mkutano na Wabunge wa Umoja wa Afrika – Japan, tarehe 29 Mei 2024.
Mhe. Seiichi Onodera, Naibu Waziri anayeshughulikia Miradi ya Kimataifa wa Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii ya Japan, Mhe. Balozi Baraka Luvanda na Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania.
Mhe. Seiichi Onodera, Naibu Waziri - Miradi ya Kimataifa wa Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii ya Japan, akifungua Semina Elekezi ya Uwekezaji kwa Jumuiya ya Japan kwa Maendeleo ya Miundombinu ya Afrika (JAIDA), tarehe 29 Mei 2024.
Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwenye Semina Elekezi ya Uwekezaji kwa Jumuiya ya Japani kwa Maendeleo ya Miundombinu ya Afrika (JAIDA), tarehe 29 Mei 2024.
Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda akifunga Semina ya Uwekezaji na Kampuni zinazohusika na Ujenzi na Miundombinu zilizo chini ya Jumuiya ya Kampuni za Japani kwa Maendeleo ya Miundombinu ya Afrika (JAIDA), jijini Tokyo, tarehe 29 Mei 2024.
Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda na Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwenye picha ya pamoja na Bw. Toshiyuki Nakamura, Mshauri Mkuu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), tarehe 29 Mei 2024.
Mazungumzo na Watendaji Wakuu na Wamiliki wa Makampuni ya KEIDANREN, jijini Tokyo, tarehe 30 Mei 2024.
Picha ya pamoja, katika Ofisi za Meya wa Jiji la Osaka, Japan, mara baada ya kuhitimisha mazungumzo na Naibu Meya wa Jiji la Osaka, tarehe 30 Mei 2024.
Picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Kampuni ya EARTH PHARMACEUTICALS, mara baada ya kuhitimishwa kwa mazungumzo, jijini Osaka, tarehe 30 Mei 2024.
Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwenye Semina Elekezi ya Uwekezaji jijini Osaka, wakati wa Kampeni ya Kuhamasisha na Kutangaza Fursa za Uwekezaji za Tanzania nchini Japan, tarehe 31 Mei 2024
Miongoni mwa washiriki kwenye Semina Elekezi ya Uwekezaji jijini Osaka, wakati wa Kampeni ya Kuhamasisha na Kutangaza Fursa za Uwekezaji za Tanzania nchini Japan, tarehe 31 Mei 2024.
Picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Kampuni ya DAIKIN kwenye Makao Makuu ya Kampuni hiyo, jijini Osaka, tarehe 31 Mei 2024.
Picha ya pamoja, katika Ofisi za Gavana wa Jimbo la Osaka, Japan, mara baada ya kuhitimisha mazungumzo na Naibu Gavana wa Jimbo la Osaka, tarehe 31 Mei 2024.
Kongamano la Uwekezaji kwa Diaspora wa Tanzania nchini Japan (Tanzanite Society) tarehe 2 Juni 2024, Ubalozini, Tokyo.
Picha ya pamoja na wawakilishi wa Kampuni ya YAMAHA kwenye Makao Makuu ya Kampuni hiyo, jijini Hamamatsu, Shizouka, tarehe 4 Juni 2024.
Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda na Bw. Kenichi Ayukawa, Makamu wa Rais wa Kampuni ya SUZUKI kwenye Makao Makuu ya Kampuni hiyo, jijini Hamamatsu, Shizouka, tarehe 5 Juni 2024.
Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda kwenye picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Kampuni ya KIKKOMAN kwenye Makao Makuu ya Kampuni hiyo, jijini Chiba, tarehe 6 Juni 2024.
Picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha Kampeni ya Kutangaza na Kuhamasisha Fursa za Uwekezaji Tanzania nchini Japan, tarehe 7 Juni 2024, Ofisi za UNIDO.