Ubalozi umepokea taarifa ya fursa za ufadhili wa masomo nchini Japan inayotolewa na Serikali ya Japan kupitia Wizara ya Elimu, Utamaduni, Michezo, Sayansi na Teknolojia (Ministry of Education, Culture, Sports, Science and Technology - MEXT) kwa mwaka wa masomo 2025. Ufadhili huo ni kwa masomo ngazi ya Shahada ya Kwanza (Undergraduate Studies), Umahiri (Master’s Degree), Uzamivu (PhD.) pamoja na Mafunzo ya Ufundi (Specialized Training College).

Taarifa zaidi kuhusu ufadhili ikiwemo, sifa na taratibu za uoambaji tafadhali pakua tovuti ifuatayo:👇🏻
https://www.tz.emb-japan.go.jp/itpr_ja/MEXT2025_000001.html