FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO NCHINI AUSTRALIA
“AUSTRALIA AWARDS SCHOLARSHIP”
Ubalozi unapenda kuwajulisha uwepo wa fursa za ufadhili wa masomo nchini Australia “Australia Awards Scholarship” kwa mwaka wa masomo 2024. Ufadhili huo ni kwa ajili ya masomo ngazi ya Umahiri (Masters Degree) kwenye masuala ya kilimo, mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula, nishati, madini, mambo ya nje na ulinzi.
Taarifa zaidi kuhusu ufadhili huo ikiwemo, sifa na taratibu za uombaji zinapatikana kupitia tovuti zifuatazo:
https://www.dfat.gov.au/people-to-people/australia-awards/australia-awards-scholarships
https://www.dfat.gov.au/about-us/publications/australia-awards-scholarships-policy-handbook
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 01 Mei 2023.
UBALOZI WA TANZANIA
TOKYO