Tarehe 8 Machi 2025, Mhe. Balozi Baraka Luvanda aliukaribisha Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki mafunzo ya usimamizi wa miradi ya jotoardhi, yanayofanyika jijini Kawasaki, Japan. Mafunzo hayo yameandaliwa chini ya mwamvuli wa Chama cha Ushirikiano wa Wataalam wa Nje na Ubia Endelevu (Association for Overseas Technical Cooperation and Sustainable Partnerships - AOTS).
Ujumbe huo umeongozwa na Dr. Khatibu Malimi Kazungu, Naibu Katibu Mkuu (Umeme na Nishati Jadidifu) wa Wizara ya Nishati; na kushirikisha wataalam kutoka Ofisi ya Rais na Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC).