Tarehe 14 Aprili 2024,  Balozi Baraka Luvanda alizindua Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa mashindano ya mpira wa miguu “MUUNGANO CUP 2024”. 

Mashindano hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano na Timu ya Mpira wa Miguu ya Diaspora wa Tanzania “The Kilimanjaro FC”, jumla ya timu 20 za Diaspora wa mataifa mbalimbali zenye uwakilishi nchini Japan, zilishiriki. 

Mashindano hayo yalifunguliwa na kufungwa na Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda ambapo, Timu ya Karisma ya Peru iliibuka kidedea kuwa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo; mshindi wa pili - Timu ya Yamato FC; na mshindi wa tatu - Timu ya ISC, zote mbili kutoka Vietnam.