Mafunzo ya Lugha ya Kiswahili yalitolewa katika Darasa la Shule ya Sekondari ya Yoga na mwenza wa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Bi. Consolata Luvanda. Mafunzo hayo yalishirikisha wanakikundi cha kijamii ya Yoga (Yoga Community Club) na kuhudhuriwa na wajapan 58 waliokuwa wamechanganyika watu wazima na watoto.

Pia, walipata maelezo kuhusu Tanzania na kuona video inayohusu Tanzania na vivutio vyake. Kikundi hicho kimeahidi kuendelea kupata mafunzo hayo na kuangalia namna nzuri ya kuyaendesha kwa kushirikiana na Ubalozi.