Tarehe 17 Aprili 2026, Ubalozi ulishiriki katika Maonesho ya AWAAJ (Association of Wives of African and Arabs Ambassadors in Japan) yanayoandaliwa na wenza wa Mabalozi wa nchi za Afrika zenye uwakilishi nchini Japan. Maonesho hayo hufanyika kila mwaka jijini Tokyo na hulenga kutangaza utamaduni, bidhaa na fursa mbalimbali kutoka nchi za Afrika.
Katika maonesho hayo, Bi. Suzana Mutatembwa, akiongozana na wenza wa watumishi wa Ubalozi, walishiriki kikamilifu katika kuonesha na kutangaza bidhaa mbalimbali za Tanzania, ikiwemo bidhaa za asili, kazi za mikono pamoja na vivutio vya utalii. Ushiriki huo uliwezesha kuongeza uelewa kwa washiriki kuhusu Tanzania kama kivutio cha utalii na uwekezaji, pamoja na kuimarisha mahusiano ya kijamii na kiutamaduni kati ya Tanzania na Japan.





