Tarehe 28/08/2026 Balozi Anderson Mutatembwa alikutana na kufanya mazungumzo na watumishi wanne (04) wa kujitolea kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) chini ya Programu iitwayo “Japan Overseas Cooperation Volunteer - JOCV”. Watumishi hao wanatarajiwa kuondoka tarehe 28 Septemba 2026 kwenda Mikoa ya Iringa, Songea na Mwanza kuhudumu katika sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii na Elimu. Mpango wa JICA kupeleka watumishi wa kujitolea nchini Tanzania ulianza Miaka 60 iliyopita ambapo hadi sasa watumishi zaidi ya 1,700 walishahudumu kwa kipindi cha miaka miwili miwili.