Leo, tarehe 9 Disemba 2024, Ubalozi uliambatana na Ujumbe wa wataalam kutoka makampuni ya chai ya Japan, Kawasaki Kiko Co. Ltd. na Nasa Corporation walioambatana na mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), kutembelea Makao Makuu ya Bodi ya Chai Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania(TBT), Beatrice Banzi amepokea ugeni huo wa wawekezaji kutoka Japan ambao utakuwepo nchini kwa siku tano ukitembelea mikoa ya Dodoma, Iringa, Mbeya na Njombe. Lengo la ziara hiyo, ni kuliongezea thamani zao la chai ya Tanzania kwa kuongeza uzalishaji, kutafutia wawekezaji na masoko ya nje ya nchi.
Ujumbe huo uliweza kuwa na mazungumzo na wadau wa chai nchini ambapo, majadiliano yalijikita katika fursa zilizopo katika zao hilo kwenye uwekezaji, masoko na kuwajengea uwezo wadau wa chai wa Tanzania.
##chaiyetufahariyetu