Wanariadha sita kutoka Tanzania wameng’ara katika Mashindano ya Mbio ndefu ya Nagai Marathon yaliyofanyika tarehe 19/10/2025. Katika mashindano hayo, Mwanariadha Michael Kishiba Sanga ameshinda nafasi ya kwanza mbio za Marathon Kilomita 42 wanaume huku Charles Boay Sulle akishika nafasi ya pili. Upande wa wanawake kilomita 42 Vaileth Adam Kidasi ameshika nafasi ya kwanza. Mbio ndefu za kilomita 21 wanawake Agnes Protas Mwaghui ameshinda nafasi ya kwanza ambapo Joseph Tiophil Panga ameshika nafasi ya pili kilomita 21 wanaume na Jumanne Maduhu Ndege ameshika nafasi ya nne.
Nagai Marathon hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka 2025 ilishirikisha wakimbiaji 1,270 wengi kutoka Japan na wachache mataifa mengine. Wachezaji wa Tanzania wameongozana na Walimu wawili ambao ni Mzee Juma Ikangaa na Samson Nyonyi.