Tarehe 03 Septemba, 2023 katika ukumbi wa Stesheni Akita nchini Japan Wanafunzi wa Kitanzania kwa kushirikiana na Ubalozi walishiriki maonesho ya Tamasha la Kimataifa la Akita yaliyoandaliwa na Mamlaka za mji huo. Maonesho hayo yalishirikisha nchi zipatazo thelasini (30) zikiwemo za Asia na Pasifiki, Afrika na visiwa vya Caribbean. Katika Banda la Tanzania wanafunzi hao Bw. Mikidadi Shaka, Bi. Mary Moshi na Bw. Bahati Kanju pamoja na Afisa ubalozi Bw. Hosea Chikolongo walionesha mavazi ya kitanzania, kuelezea vivutio mbalimbali vya utalii pamoja na vyakula na kugawa majarida na vipeperushi kwa washiriki na kugonga muhuri wa Tanzania wenye picha ya Mlima Kilimanjaro katika mfano wa Hati za kusafiria walizogawiwa watu mbalimbali waliofika katika maonesho hayo. Aidha wanafunzi hao walipita jukwaani kuonesha vazi la kimasai na baadae kucheza ngoma za kiafrika pamoja na wenzao.