Tarehe 27 Oktoba 2023, Balozi Baraka Luvanda alitembelea Ofisi za Kampuni ya Baraka iliyopo Osaka, inayomilikiwa na Bw. na Bibi. Tsuyoshi Shimaoka, wajapani wenye makazi na biashara, Zanzibar kwa zaidi ya miaka 30. 

Kampuni hiyo inatengeneza na kuuza bidhaa za utamaduni wa Tanzania nchini Japan ikiwemo, kanga, vitenge, vinyago, picha za kuchora za tingatinga, urembo uliotengenezwa kiutamaduni; na bidhaa za vyakula kama vile korosho, tende, kahawa, chai na viungo (spices) kutoka Zanzibar.