Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda amepokea Ujumbe wa wanafunzi wa Chuo Kikuu SOKA uliokuja kutoa mwaliko kwa Mhe. Balozi kuwa Jaji Mkuu wa Mashindano ya 34 ya Hotuba ya Lugha ya Kiswahili katika Chuo hicho.

Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Klabu ya Urafiki ya Pan African (Pan African Friendship Society) ya Chuo Kikuu SOKA katika kuenzi mchango wa MWASISI WA CHUO KIKUU CHA SOKA, DK. DAISAKU IKEDA katika kuimarisha ushirikiano wa Kimataifa.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba, Chuo Kikuu SOKA, jijini, Tokyo, na kushirikisha Wajapani wanaozungumza lugha ya Kiswahili.