Wanariadha sita kutoka Tanzania wameng'ara katika mashindano ya mbio ndefu ya Nagai marathon kwa mwaka 2026 yaliyofanyika tarehe 18/10/2026 katika mji wa Nagai uliopo Mkoa wa Yamagata, Japan.
Katika mbio hizo, mwanariadha Michael Kishiba Sanga ameshinda nafasi ya kwanza kwa wanaume Kilomita 42 huku Charles Boay Sulle akishika nafasi ya pili. Upande wa wanawake kilomita 42 nafasi ya kwanza imechukuliwa na Vaileth Adam Kidasi. Mbio za kilomita 21 wanaume Fabian Nelson Sulle ameshika nafasi ya kwanza na Joseph Tiophil Panga ameshika nafasi ya pili. Upande wa wanawake kilomita 21 Agnes Protas Mwaghui ameshinda nafasi ya kwanza.
Katika mbio za Nagai Marathon za mwaka huu, jumla ya washiriki 1,411 walijiandikisha na kushiriki. Kati yao 812 marathon kilomita 42, washiriki 337 kilomita 21 na wakimbiaji 262 ni kawaida.





