Balozi wa Tanzania nchini Japani, Mhe. Anderson G. Mutatembwa, akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Kampuni ya Dai Nippon Printing (DNP), Bw. Satoshi Shimizu na Bw. Koichi Kishi, baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ubalozini Tokyo, leo tarehe 9 Oktoba 2026.

Mazungumzo hayo yalijikita katika fursa za ushirikiano kwenye teknolojia za utambuzi na mifumo ya kidijitali, ikiwemo vitambulisho vya Taifa, hati za kusafiria, leseni za udereva na mifumo mingine inayochangia kuboresha huduma za umma na kukuza uchumi wa kidijitali.

Pande zote zilikubaliana kuendeleza mazungumzo kupitia kikao cha mtandao kati ya kampuni hiyo na taasisi husika za Tanzania, kitakachoratibiwa na Ubalozi, kwa lengo la kuchunguza fursa za ushirikiano na uhamishaji wa teknolojia.

#DiplomasiaYaUchumi #TanzaniaJapan #DigitalTransformation #TechnologyTransfer