Tarehe 13 Oktoba 2026 Balozi Anderson Mutatembwa alitembelea kampuni ya Product Planning Relations (PPR) inayomilikiwa na Bw. Sanata Mitsuyasu katika mji wa Takasaki, Mkoa wa Gunma nchini  inamiliki mkusanyiko wa picha za Tingatinga 320 ambazo ni sanaa yenye asili ya Tanzania.

Katika ofisi yake Bw. Sanata alionesha picha za sanaa ya Tingatinga za miaka mingi hususan kuanzia miaka ya 1984 zilizochorwa na wasanii mbalimbali wa Tanzania na kuonyesha nia yake ya kutaka picha hizo zirejeshwe Tanzania na kuhifadhiwa katika Makumbusho maalum.

Baada ya kuona picha hizo, Balozi Mutatembwa aliahidi ubalozi kuanzisha mazungumzo na mamlaka zinazohusika ili kufikia makubaliano yatakatowezesha picha hizo kurejeshwa Tanzania na kutengenezewa Makumbusho maalum ili kulinda na kuhifadhi historia yake.